WAVUJAJASHO DHIDI YA SOKO HURIA

WAVUJAJASHO DHIDI YA SOKO HURIA

WAVUJAJASHO DHIDI YA SOKO HURIA

(Swahili below)

From the early 1970s, the capitalist system changed and started taking the free market face. Free market capitalism was introduced to rob power, authority, resources, and profits from the hands of workers and put them in the hands of capitalists. Every respite for the workers through free social services was removed and put in the hands of capitalists.

But workers have not agreed with this system that takes them back to slavery. They have been fighting to minimize its effects, to bury it and build alternatives. Articles in this publication show workers’ experiences in the free market system, their struggles against it and their visions of an alternative system that is founded on humanity, equality, and justice.

***********************************************

Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1970 mfumo wa kibepari ulianza kubadilika na kuchukua sura ya Soko Huria. Ubepari wa Soko Huria uliletwa kwa ajili kupora nguvu, mamlaka, rasilimali na faida kutoka mikononi mwa wavujajasho na kuviweka mikononi mwa mabepari. Unafuu wowote uliokuwa umetolewa kwa wavujajasho, hasa kupitia huduma za jamii zisizo na malipo, uliondolewa na kurejeshwa mikononi mwa mabepari.

Lakini wavujajasho hawajakubaliana na mfumo huu unaozidi kuwarejesha utumwani. Wamekuwa wakipambana kupunguza makali yake, kuuzika na kujenga mbadala. Makala zilizokusanywa katika kitabu hiki zinaelezea uzoefu wa wavujajasho ndani ya mfumo wa Soko Huria, namna wanavyopambana nao, na maono yao juu ya mfumo mbadala unaozingatia utu, usawa na haki.

Click Here to Download Publication 

Close